
Tarehe 11 Julai 2022 – 31 Oktoba 2023
Tazama ukurasa huu kwa Kiingereza, Kifaransa au Kiarabu.
Dhamira ya Shirika la African Alliance ni kuwa na ulimwengu ambao watu wanaokosa haki na wahanga wa matumizi mabaya ya madaraka wanaweza kuhakikishiwa kwamba kuna watu watakaosimama nao katika juhudi za kujenga jamii inayojali usawa na haki duniani na yenye kuonesha upendo mkubwa katika kutetea, kuhifadhi, kulinda sambamba na kutanua wigo wa haki zao na za watu wengine. Tumekusudia kuendeleza miradi nyeti inayohamasisha, na kuendeleza haki katika kukabiliana mahitaji ya jamii zilizotelekezwa kote barani Afrika kwa kushirikiana katika kuhakikisha kwamba wanajamii wanaonyanyaswa wanaelimishwa kuhusu haki zao, wanapata huduma za afya ya dharura zenye kulinda utu wao sambamba na kuwawajibisha watendaji pale ambapo haki hizi hazipatikani.
Muungano wa Chanjo ya Watu ni muungano wa mashirika na mitandao zaidi ya 90, inayosaidiwa na Washindi wa Tuzo ya Nobel, wataalam wa afya, wachumi, Wakuu wa Nchi, viongozi wa kidini na wanaharakati, wanaoshirikiana katika kufanikisha kampeni ya Chanjo ya Watu, inayotolewa kwa kila mtu bila gharama yoyote, sehemu yoyote ile.
Katika kutambua umuhimu huu – hali ambayo imedhirika kupitia janga hili – tumedhamiria kutafuta suluhu za ndani katika mifumo inayokabiliana na janga hili, kuhakikisha kwamba sauti za Waafrika zinasikika na vipaumbele vyetu vinawekewa msisitizo na kuongeza hamasa, shirika la African Alliance limekuwa jukwaa muhimu ambalo programu ya Muungano wa Chanjo Barani Afrika inatekelezwa. Muungano huu unaosimamiwa kutoka kanda zote tano za bara hili ambapo uenyekiti wake unashikiliwa ni shirika la African Alliance, kazi hii kubwa inayofanywa na Muungano wa Chanjo ya Watu inatumia suluhu kutoka ndani ya Afrika, na inatekelezwa na viongozi wa kanda mbalimbali sambamba na kusimamiwa na mkakati wa kimataifa wa Muungano wa Chanjo ya Watu.
Shirika la African Alliance lina furaha kubwa kualika mashirika ambayo yana sifa zilizotajwa hapa chini kutuma maombi ya kupata ruzuku kama Wanufaika wa Ruzuku.
Mchakato wa kuchambua maombi utasimamiwa na Kamati ya Uendeshaji ya PVA, ambayo inaundwa na wawakilishi wa mashirika ya uraia kutoka kila kanda ya Afrika.
Ruzuku 2 za thamani ya ZAR 280 000 kwa kila moja katika kipindi chote cha mradi huu
Ruzuku 2 za thamani ya ZAR 280 000 kwa kila moja katika kipindi chote cha mradi huu
Ruzuku 2 za thamani ya ZAR 280 000 kwa kila moja katika kipindi chote cha mradi huu
Ruzuku 2 za thamani ya ZAR 280 000 kwa kila moja katika kipindi chote cha mradi huu
Ruzuku 2 za thamani ya ZAR 280 000 kwa kila moja katika kipindi chote cha mradi huu
Kumbuka kwamba miradi hii si lazima itekelezwa katika kipindi chote cha ruzuku hii (Tarehe 1 Julai, 2022 – Tarehe 31 Oktoba31 2023) lakini inaweza kutekelezwa katika ndani ya muda mfupi.
Unaweza kushirikiana na mashirika mengine yanayopatikana katika kanda yako. Lakini unaruhusiwa kushirikiana na shirika moja pekee. Hata hivyo, ni shirika moja pekee (mwombaji mkuu wa ruzuku) ndilo litakalopewa ruzuku na ndilo litakalokuwa na wajibu wa kutuma ripoti za kazi iliyofanywa.
Ikitokea kwamba pendekezo moja kutoka kanda fulani limeshinda, Kamati ya Uendeshaji ina haki ya kutoa ruzuku yote ya kanda kwa mwombaji huyo pekee katika kanda yote.
Ni waombaji ambao maombi yao yataoorodheshwa pekee ndio watakaoalikwa kuendelea na hatua zinazofuata.
Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Mei 2022. Tunahimiza kwamba utume maombi mapema kwa sababu hatutapokea maombi kupitia mfumo wa mtandaoni baada ya tarehe ya mwisho na maombi yatakayotumwa kwa njia ya barua pepe hayatakubalika.
Kando na kikao cha mtandaoni (Webinar) cha tarege 19 Mei 2022, unaweza kutuma maswali kwa granteesupport@africanalliance.org.za hadi tarehe 26 Mei 2022. Majibu ya maswali haya yatakusanywa na kuchapishwa hapa na tutaendelea kuyajibu kadri tutakavyopokea maswali hadi siku ya mwisho.